UTARATIBU WA KUWEKA CHUMBA CHA KUPIKIA(KITCHEN)



Habari za wakati mpendwa msomaji! Karibu tena kwenye uwanja huru wa kujipatia taarifa na elimu mbadala kwa mambo ya ujenzi.

Mpendwa msomaji utaratibu wa kuweka chumba cha kupikia (kitchen) kwenye nyumba ya kuishi(residential) ulianza kuzingatiwa zaidi miaka ya 1920s na katika nchi zetu za kiafrika miaka ya 1970s japo mpaka sasa bado kuna baadhi ya maeneo haujazingatiwa. Utaratibu huu ulianzishwa hasa maeneo ya mijini kwa lengo la kupunguza matumizi ya eneo yasiyokuwa ya lazima na kwa ajili ya ulinzi(security and privacy).


Chumba cha kupikia(kitchen) ni chumba chenye pilika pilika (movement) nyingi karibia robo tatu siku (imekadiriwa kwamba mtu anayeandaa chakula kwenye chumba kisicho na mpangilio mzuri movement anazofanya ni sawa na mtu aliyetembea maili moja na nusu), hivyo basi ni vizuri kuweka mpangilio mzuri ili kupunguza pilika pilika(movement) zisizokuwa na msingi.

Kumbuka : tupo wataalamu tuliobobea kwenye mambo ya upangiliaji wa ndani ya nyumba (interior designer) hivyo basi kama itakusumbua ni vizuri kututafuta wataalamu husika tukusaidie
                                                                                           
Vitu vya msingi kuwepo kwenye chumba cha kupikia (kitchen)
Ili twende sawa kwenye hiki chumba kuna maeneo matatu (3) ya msingi kuzingatiwa. Mwisho utaona picha kwa vielelezo.
1. sehemu ya kuhifadhi(preservation & storage) – Eneo hili ni vizuri kuwa karibu na mlango wakutokea ili iwe rahisi mtu akiingia tu anaweka vitu, katika nyumba kubwa hili eneo pia hutafutiwa chumba chake. Hapa kuna vitu vifuatavyo
  • Jokofu (refrigerator)
  • makabati (shelves or cupboard)
2. Sehemu ya maandalizi na usafishaji(preparation & cleaning) – Hapa ndiyo maandalizi ya vifaa vya kupikia pamoja na malighafi za mapishi zinapoandaliwa, ni vizuri kuwa karibu na dirisha. Vitu vinavyotakiwa kuwepo;
  • Meza (table)
  • Sink
3. Sehemu ya kupikia (cooking center) – hii ndiyo sehemu ya kutayarishia chakula, vitu vinavyotakiwa kuwepo;
  • jiko la kupikia (stove or range)
  • kabati la juu (shelves)
Picha za vielelezo


USIPITWE!! Endelea kuwa nasi kwa taarifa nyingine kuhusu ujenzi.Ahsante

Comments