USHAURI

                                   

                                JINSI YA KUJENGA NYUMBA  YAKO SEHEMU YENYE MWINUKO


Habari za wakati mpendwa msomaji wa makala hizi za ujenzi! Lengo letu ni kuhakikisha unaendelea kutembelea mtandao huu kwa kujifunza mambo mbalimbali ya ujenzi
Katika ujenzi kiwanja ni kipande cha eneo ambacho hutumika kwa kujenga majengo mbalimbali. viwanja hutofautiana  kutoka eneo moja hadi lingine kulingana na sura ya eneo husika kama vile bondeni, milimani na tambarare.
Katika viwanja vilivyopo kwenye maeneo yaliyoinuka hususani milimani ujenzi wake huwa tofauti katika msingi(foundation) tofauti na maeneo mengine.
Kuna vitu viwili vya kuzingatia kwa wale wanaotaka kujenga kwenye viwanja vilivyopo kwenye miinuko (slope).
1. Kujenga kwa ngazi(steps) – hii ni aina ya kujenga kwa kufuata usawa (level) ya vieneo vinavyounganisha eneo zima.


2. Kujenga kwa kuchimba/kujaza – hii ni aina ya ujenzi ambayo wajenzi huchimba/kujaza udongo kwa lengo la kusawazisha kisha kuendelea na ujenzi.

Muhimu: Unapofikiria kutengeneza ramani ya kujenga ni vyema kuzingatia hili kwa sababu unaweza kuwa na ramani nzuri lakini isijengeke kwenye kiwanja chako.

Comments